Matumaini ya United kumnasa mshambuliaji wa Atletico Antonio Griezman yayeyuka




Ndoto za Mashetani wekundu kuinasa saini ya Mfaransa Antonio Griezman zimeyeyuka baada ya FIFA kuifungia Atletico Madrid  kusajili mchezaji hadi mwaka 2018.

Atletico Madrid wamefungiwa kusajili  na FIFA baada ya kukutwa na kosa la kuvunja sheria ya uhamisho wa mchezaji chini ya umri wa miaka 16.

Kutokana na katazo hilo la FIFA Atletico Madrid wamesema hawatakuwa tayari kumruhusu nyota wao kujiunga na timu yeyote katika uhamisho wa majira haya ya joto hivyo kukatiza kiu ya Man U kumtwaa mshambuliaji huyo.

Baada ya FIFA kutoa taarifa hizo Griezman aliandika ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram ukisema anataendelea kubaki na Atletico Nadrid msimu ujao.

Atletico Madrid wanajiandaa kumsainisha mkataba mpya nyota huyo ilikuzuia uwezekano wa timu za Ulaya kumpata Mfaransa huyo.


Ozil kusaini mkataba mpya



Kiungo wa Arsenal Mesut Ozil anatarajiwa kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Arsenal siku chache zijazo baada ya nyota huyo kufikia  makubaliano ya malipo ya mshahara na Arsenal.

Nyota huyo raia wa Ujerumaini alionekana kama ataihama Arsenal majira haya ya joto ama mwishoni mwa mwaka 2018 ambapo mkataba wake ndo unamalizika kutokana na mazungumzo ya awali kushindwa kufikia muafaka lakini sasa nyota huyo amekubali kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.

Ozil amekubali malipo ya paundi 280000 kwa wiki licha ya hapo awali kudai pesa nyingi zaidi ya hizo ilikusaini mkataba mpya.

Arsenal wanamatumaini pia ya kumshawishi nyota wao Alexis Sanchez kusaini mkataba mpya baada ya mwenzake Ozil kukubali kubaki Emirates.

Manchester City yakamilisha uhamisho wa beki Benjamin Mendy kutoka Monaco


Manchester City wamekamilisha dili la beki Benjamin Mendy kutoka Monaco kwa dau la £39.8 millioni kwa mujibu wa taarifa kutoka The Sun.

Beki huyo raia wa Ufaransa amesaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo ya Manchester City ambapo atakuwa akipokea mshahara wa  £100,000 kwa wiki.

Mendy mwenye umri wa miaka 22 atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa kutoka Monaco baada ya Bernado Silva kujiunga na City siku chache zilizopita kwa ada ya £43 millioni.

Beki huyo ambaye anaitumikia timu ya taifa ya Ufaransa kwa sasa atakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na pep Guardiola baada ya kocha huyo kuwanasa kipa Ederson kutoka Benfica na Bernado Silva ambaye alisajiliwa kutoka Monaco.

Mendy anatarajiwa kusaini mkataba rasmi akimaliza majukumu yakuitumikia timu yake ya taifa ya Ufaransa mechi za kimataifa ambapo usiku wa leo wanacheza na Paraguay huku tarehe 9 wakitarajia kuumana na Sweeden huku tarehe 13 wakitarajiwa kuikarisha England.

Manchester City yaipiga bao Man U kwa Bernado Silva


Manchester City wamekamilisha usajili  wa Bernado Silva kutoka As  Monaco kwa mkataba wa miaka mitano kwa mujibu wa taarifa kutoka Daily Mail.

City walikuwa wakichuana na United katika mbio za kuiwania saini ya nyota huyo wa kimataifa kutoka Ureno lakini City wameipiga bao klabu ya Manchester United baada ya kumnasa nyota huyo kwa kitita cha pauni millioni 43.

Bernado Silva aling'ara msimu uliomalizika hivi karibuni akiwa na Monaco akiifungia klabu hiyo mabao 11 na kutoa pasi 12 za mabao.

Silva mwenye umri wa miaka 22 atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Pep Guardiola katika majira haya usajili kwani kocha huyo anataka kukijenga upya kikosi cha City.

Guardiola anataka kuimarisha kikosi chake ilikurudisha heshima yake ya kutwaa mataji katika timu zote alizopita baada ya msimu huu kumalizika bila taji lolote.

Mourinho aipa masharti magumu Real Madrid kwa De Gea


Kocha wa Manchester United Jose Mourinho ameitaka klabu ya Madrid kutoa kitita cha pauni millioni 25 pamoja na mshambuliaji Alvaro Morata kama inania ya kumpata kipa huyo kwa mujibu wa The Mirror.

De Gea amekuwa akiwindwa na timu hiyo ya Real Madrid kwa mda mrefu na huenda safari hii akatimkia Madrid kutokana na kocha wa sasa wa United kuonekana kuanza kumwamini kipa namba mbili wa timu hiyo
Romelo.

Aubemayang kuondoka Dortmund


Mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubemayang ameomba kuihama klabu hiyo katika majira ya uhamisho wa majira ya joto.

Mshambuliaji huyo raia wa Ghabon hatajatoa maamuzi yake kuhusu timu gani anaenda lakini timu za PSG,Ac Milan na Tianjin Quanjian zinamtaka nyota huyo.

Dortmund wameshaanza kumsaka Patrik Schichk kama mridhi wa nyota huyo.

Claude Makelele asaini mkataba mpya kuendelea kubakia Swansea City kama kocha msaidizi


Kiungo wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa Claude Makelele amasaini mkataba mpya wakuendelea kubaki katika timu ya Swansea City kama kocha msaidizi.

Makelele ambaye jina lake ni maarufu sana kwa wapenzi wengi wa soka kulingana na umahiri wake uwanjani aliwahi pia kuzichezea klabu za Real Madrid na Paris Saint-Germain.

Makelele mwenye umri wa miaka 44 alijiunga na Swansea City kwa mda majira ya January baada ya Paul Clement kuchaguliwa kuwa kocha wa timu hiyo.


Arsenal wanamtaka Thorgan Hazard


Arsenal wanataka kumsajili winga wa Borrussia Monchengladbach Thorgan Hazard katika uhamisho wa majira ya joto.

Kinda huyo ambaye ni mdogo wake na Eden Hazard wa Chelsea amewavutia Arsenal baada ya kuonesha kiwango maridadi msimu huu akiwa na Monchengladbach.

Taarifa kutoka chanzo kimoja cha habari cha Jeunes Footeux zimebainisha kuwa Arsenal watalazimika kutumia kitita cha uero millioni 18 ilikumpata kinda huyo.

Simon Msuva,Kaseke na Kaseke kufungiwa kucheza mechi za ligi kuu ya Tanzania



Wachezaji watatu wa Yanga Simon Msuva,Deus Kaseke pamoja Obrey Chirwa wamefungiwa kucheza mechi za Ligi kuu Tanzania bara baada ya kufanya vurugu katika mchezo kati ya Yanga na Mbao Fc.

Katika mchezo huo uliopigwa Mei 20 mwaka huu katika uwanja wa CCM Kirumba wachezaji hao watatu walimsukuma na kumwangusha mwamuzi wa mchezo huo Ludovic Charles jambo ambalo lilizua ugomvi katika mchezo huo.

Wachezaji hao watalazimika kusubiri maamuzi ya kamati ya maadili ya TFF kuhusu hatma yao kujua endapo wataruhusiwa kuendelea kuitumikia Yanga katika mechi za ligi kuu Tanzania bara.

Arsenal wamtengea dau nono Sanchez



Arsenal wemtengea mezani nyota wao Alexis Sanchez kitita cha pauni  270 000 kwa wiki ilikumshawishi kuendelea kubaki Emirates.

Arsenal wamemuwekea nyota huyo kitita hicho kinono cha pesa ilikuzuia klabu zinazo mnyemelea kumpata winga huyo.

Licha ya Arsenal kuweka kitita hicho Alexis mwenyewe anataka kulipwa pauni 300000 kwa juma lakini Arsenal wamemwambia watakuwa tayari kumpa malupulupu nje na mshahara waliomtengea.

Timu nyingi za Ulaya zimekuwa zikivutiwa na nyota huyo wa kimataifa kutoka Chile kulingana na uwezo wake wa kusakata soka hivyo Arsenal wanatalazimika kutumia mbinu zote ilikumshawishi kubaki hapo.