Matumaini ya United kumnasa mshambuliaji wa Atletico Antonio Griezman yayeyuka




Ndoto za Mashetani wekundu kuinasa saini ya Mfaransa Antonio Griezman zimeyeyuka baada ya FIFA kuifungia Atletico Madrid  kusajili mchezaji hadi mwaka 2018.

Atletico Madrid wamefungiwa kusajili  na FIFA baada ya kukutwa na kosa la kuvunja sheria ya uhamisho wa mchezaji chini ya umri wa miaka 16.

Kutokana na katazo hilo la FIFA Atletico Madrid wamesema hawatakuwa tayari kumruhusu nyota wao kujiunga na timu yeyote katika uhamisho wa majira haya ya joto hivyo kukatiza kiu ya Man U kumtwaa mshambuliaji huyo.

Baada ya FIFA kutoa taarifa hizo Griezman aliandika ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram ukisema anataendelea kubaki na Atletico Nadrid msimu ujao.

Atletico Madrid wanajiandaa kumsainisha mkataba mpya nyota huyo ilikuzuia uwezekano wa timu za Ulaya kumpata Mfaransa huyo.