Arsenal yatengewa pauni million 85 kuwaachia Giroud na Koscielny

Olympique Marseile inawafukuzia nyota wawili wa Arsenal Olivier Giroud pamoja na beki wakati Laurent Koscielny taarifa kutoka L'Equipe zinaripoti.

Marseile wamesema wako tayari kutoa kitita cha pauni millioni 85 kuwanasa wawili hao katika majira ya joto wakiwa wanataka kurejesha hadhi yao iliyopotea kwa mda mrefu katika soka la Ufaransa na Ulaya pia.