Manchester City wamekamilisha dili la beki Benjamin Mendy kutoka Monaco kwa dau la £39.8 millioni kwa mujibu wa taarifa kutoka The Sun.
Beki huyo raia wa Ufaransa amesaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo ya Manchester City ambapo atakuwa akipokea mshahara wa £100,000 kwa wiki.
Mendy mwenye umri wa miaka 22 atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa kutoka Monaco baada ya Bernado Silva kujiunga na City siku chache zilizopita kwa ada ya £43 millioni.
Beki huyo ambaye anaitumikia timu ya taifa ya Ufaransa kwa sasa atakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na pep Guardiola baada ya kocha huyo kuwanasa kipa Ederson kutoka Benfica na Bernado Silva ambaye alisajiliwa kutoka Monaco.
Mendy anatarajiwa kusaini mkataba rasmi akimaliza majukumu yakuitumikia timu yake ya taifa ya Ufaransa mechi za kimataifa ambapo usiku wa leo wanacheza na Paraguay huku tarehe 9 wakitarajia kuumana na Sweeden huku tarehe 13 wakitarajiwa kuikarisha England.