Chelsea yakwaa kisiki kwa Andrea Belloti

Chelsea imegonga mwamba katika harakati zake za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Torino Andrea Belloti.

Chelsea walikuwa wameitengea Torino kitita cha uero millioni 51 na bonus ya uero millioni 34 jumla ikiwa euro 85 kwa ajili ya kumnasa Belloti lakini dau hilo limekataliwa na Torino.

Belloti amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu akiongoza kuzifumania nyavu katika ligi ya Serie A akiwa na magori 24 hadi sasa.

Nyota huyo wa kiitaliano anawindwa na klabu nyingi za Ulaya lakini Torino wanaonekana kutokuwa tayari kumwachia nyota wao huyo.