Serengeti Boys kuwavaa Niger leo katika mchezo wa mwisho wa Afcon U-17 hatua ya makundi


Vijana wa timu ya taifa chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys leo watashuka dimbani kupepetana na vijana wenzao kutoka Niger katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi mashindano ya AFCON U-17.

Serengeti Boys wako nafasi ya pili katika kundi B wakiwa wamelingana kwa kila kitu na timu ya kwanza  ya Mali,timu zote zikiwa na point 4,mabao 2 ya kufunga na 1 la kufungwa kila moja.

Serengeti Boys wanatakiwa kupata matokeo ya sare ya aina yoyote ile au kushinda ilikutinga hatua ya nusu fainali na pia kujihakikishia nafasi ya kushiriki kombe la Dunia kwa vijana wa umri wa miaka 17 miezi michache ijayo.

Serengeti Boys wameshuka dimbani mara mbili katika mashindano haya, mchezo wa kwanza wakitoka sare na mabingwa watetezi Mali na kuwafunga vijana wa Angola 2-1 katika mchezo wa pili.

Mashindano haya yanajumla ya makundi mawili A&B yenye timu nne nne kila moja,kundi A lilikuwa na timu za Ghana, Guinea,Cameroon pamoja na wenyeji Gabon ambapo Ghana na Guinea wakiwa wamefuzu hatua ya nusu fainali Ghana akimalimaliza wa kwanza kwa jumla ya alama 7 huku  Guinea wakimaliza nafasi ya pili kwa pointi 5,Cameroon  nafasi ya tatu wakiwa wamejikusanyia point 4 na wenyeji Gabon wakifunga mkia wakiwa hawana pointi hata moja.

Cameroon na Gabon wameaga mashindano hayo hivyo timu zingine mbili zitakazo ungana pamoja na Ghana na Guinea zitapatikana baada ya michezo ya leo