Inasemekana kuwa Sanchez amekubali kubaki Emirates hadi 2018 lakini akiwapa masharti viongozi wa klabu hiyo kufanya usajili mkubwa majira ya joto kama wanataka asaini mkataba mpya.
Bosi wa Arsenal Arsene Wenger anamatumaini kuwa nyota huyo atasaini mkataba mpya baada yamazungumzo na nyota huyo kuonekana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa baada ya hapo awali kushindikana kutokana na kutofikia muafaka wa pesa aliyokuwa akitaka kuongezewa nyota huyo.