Kingley Coman azigonganisha Chelsea na Man city

Klabu za Chelsea na Man city zimeingia katika vita ya kutaka kumsajili winga wa Bayern Munich Kingley Coman.Coman alijiunga na Bayern Munich kwa mkopo akitokea Juventus ya Italy mwaka 2015.Licha ya klabu hizi kutoka Uingereza kuonyesha nia ya kumsajili winga huyo wa kimataifa wa Ufaransa klabu ya Bayern Munich ndo inapewa nafasi kubwa  ya kumsajili kinda huyo mwenye umri wa miaka 20 kama itaamua kumbakiza Allianz Arena.Pamoja na kutakiwa na klabu hizo Coman anaweza akarejea katika timu yake ya Juventus mwishoni mwa msimu huu endapo uhamisho wake hautakamilika.