Mabingwa watetezi wa ligi kuu England leicester city jana walifanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali klabu bingwa barani ulaya baada ya kuifunga sevilla 2-0 katika uwanja wake wa nyumbani King Power stadium.Leicester City walienda mapumziko wakiwa mbele kwa gori moja lilifungwa na Wes Morgan katika dakika ya 27 ya mchezo huo huku gori la pili likipatikana dakika ya 54 kupitia kwa Marc Albrighton.
Leicester imefuzu kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya mechi ya mkondo wa kwanza kufungwa 2-1 nyumbani kwa sevilla.
Mechi nyingine iliyochezwa hapo jana iliwakutanisha miamba wa soka kutoka Italy na Fc Porto ya Ureno ambapo Juve walifanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 nakutinga hatua ya robo fainali kwa jumla ya mabao 3-0 mabao mawili ikishinda katika mechi ya mkondo wa kwanza nyumbani kwa Porto