Tundu Lissu ashinda urais wa TLS kwa asilimia 88%

Uchaguzi wa kumpata rais na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama cha wanasheria Tanganyika  Law Society(TLS) umefanyika siku ya leo jijini Arusha na wajumbe wa mkutano huo kumchagua mbunge wa singida mashariki na mwanasheria mkuu wa chadema Tundu Lisu kuwa rais wa chama hicho.Katika uchaguzi huo kura zilizopigwa zilikuwa 1682 huku Tundu Lisu akipata kura 1411 sawa na asilimia 88% ya kura zote.
Matokeo ya Urais yalikuwa kama ifuatavyo
1:Tundu Lisu kura 1411 kati ya kura 1682 zilizopigwa sawa na asilimia 88%
2:Victoria Mandali 176
3:Fransis Stolla 64 na
4:Godwin Mwapongo 64
Nafasi ya makamu wa rais imechukuliwa na aliyekuwa mwanasheria wa shirika la umeme Tanzania TANESCO bwana Godwin Ngwilimi.