Zanzibar yajitenga rasmi na Tanzania bara kimichezo

Visiwa vya Zanzibar hapo jana viliweza kupata rasmi uanachama wa CAF na FIFA baada ya wajumbe waliokuwa wakishiriki katika uchaguzi wa rais wa CAF mjini Addis Ababa kupiga kura ya kukubali ombi la Zanzibar.Zanzibar sasa itakuwa mwanachama wa 55 wa CAF na itakuwa imejitenga rasmi kimichezo na Tanzania bara katika mashindano yanayohusisha timu za mataifa ya Afrika ikilinganishwa na hapo awali ambapo Zanzibar ilikuwa ikiungana na Tanzania bara katika michuano ya kimataifa na kuunda timu moja.Katika mkutano huo pia rais wa mda mrefu wa CAF Issa Hayatou kutoka Cameroon alishindwa kutetea kiti chake alichokikalia kwa miaka 29 aliposhindwa na Ahmed kutoka Madagascar.Katika uchaguzi huo Issa Hayatou alipata kura 20 huku bwana Ahmed akipata kura 34