Arsenal kufukuzia saini ya Kingsley Coman

Arsenal wapo katika mazungumzo na klabu ya Juventus kuhusu upatikanaji wa nyota wake Kingsley Coman anayechezea Bayern Munich kwa mkopo.

Taarifa kutoka Terefoot zinaripoti kuwa Arsenal wanafanya mawasiliano na Juventus kuona kama watafikia muafaka wa kumpata nyota huyo katika uhamisho wa majira ya joto.

Coman alitolewa kwa mkopo na Juve kwenda Bayern mwaka 2015 lakini atakuwa sokoni majira ya joto na huenda akatimka Bayern baada ya vilabu vingi vya Ulaya kuvutiwa naye.