Arsenal kumtia kitanzi Jack Wilshere


Arsenal wapo katika mchakato wa mazungumzo ya mkataba mpya na nyota wake Jack Wilshere kabla mkataba wake wa sasa haujafikia tamati.

Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza kwa sasa  anakipiga katika klabu ya Bournemouth kwa mkopo na Arsenal wameanza mazungumzo naye ilikuhakikisha wanambakiza Emirates.

Mkataba wa sasa wa nyota huyo unaisha 2018 na amewataka mabosi wa Arsenal kumhakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza kabla hajasaini mkataba mpya.