Costa hatarini kupewa adhabu na FA


Mshambuliaji wa Chelsea ameingia matatani baada yakuonekana akimpiga teke beki wa Man City Vicent Company katika mechi iliyochezwa jumatano ya tarehe 5 katika  dimba la Stamford Bridge nyumbani kwa Chelsea.

Costa alionekana akimpiga teke beki huyo makusudi lakini hakuoneshwa kadi nyekundu na refa wa mchezo huo kutokana na mwamuzi kutoona  tukio hilo lakini video zilionesha kuwa Costa alimchezea rafu mbaya beki huyo.

Tukio la Costa linafananishwa na la mshambuliaji wa Man U Zlatan Ibrahimovic alipokutwa na hatia ya kumchezea vibaya mchezaji  Tyrone Mings wa FC Bournemouth lililopelekea nyota huyo kufungiwa mechi tatu na shirikisho la soka la Uingereza FA.

Costa huenda akakupambana na adhabu ya kukosa michezo mitatu sawa  na adhabu aliyopewa Ibrahimovic endapo atapatikana na hatia hizo wakati huu FA wakiwa bado wanaendelea kuchunguza tukio alililofanya mshabuliaji huyo.