Ratiba ya mechi za nusu fainali kombe la FA inatarajiwa kuendelea april 22 na 23 pale ambapo itashuhudiwa miamba ya soka la uingereza ikichuana vikali hatua hiyo.Timu zilizofuzu hatua hiyo ni Chelsea,Tottenham,Arsenal pamoja na manchester city.
Chelsea wamepangwa kucheza na Tottenham huku Arsenal wakipangwa kuchuana na Manchester City.
Tottenham walifanikiwa kufuzu hatua hiyo baada ya kuifunga Millwal 6-0 na pia wataingia kupambana kuhakikisha wanatwaa taji hilo baada yakulikosa kwa mda mrefu wakifanya hivyo mara ya mwisho mwaka 1991.
Arsenal waliwatoa Lincoln City kwa jumla ya mabao 5-0 huku Chelsea wakifuzu baada ya kuifunga Manchester United 1-0 katika mechi iliyochezwa Stamford Bridge