Kocha mkuu wa Taifa stars atangaza kikosi kipya

Koch mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania  Taifa Stars Salum Mayanja ametangaza kikosi kipya kinachoundwa na wachezaji 26 huku akiwatema baadhi ya wachezaji kutoka kikosi cha awali.
Mayanja awewaacha mabeki kazaa kutoka klabu za Yanga na Azam ambao ni Juma Abdul,Kelvin Yondan na Mwinyi Hajji Mngwali wote kutoka Yanga huku Agrey Mosses na David Mwantika wakiachwa kwa upande wa Azam.
Pia baadhi ya wachezaji kutoka Zanzibar wameachwa kwa mda katika kikosi hicho huku kukisubiriwa mkutano wa shirikisho la soka la Afrika CAF kuona kama utaweza kuipa Zanzibar uanachama.
Ikiwa Zanzibar itapewa uanachama wa CAF basi wachezaji hao hawatatumika tena katika Timu ya Taifa Stars na badala yake watajuishwa katika kikosi cha Zanzibar.
Wachezaji wlioongezeka katika kikosi hiki ni washambuliaji Mbarak Yussuf kutoka kagera sugar pamoja na Abdulrahman Juma kutoka Ruvu shooting.
Kikosi kizima kinaundwa na wachezaji wafuatao:
Makipa ni Aishi Manula (Azam),Deogratius Munishi(Yanga) na Said Mohammed kutoka Mtibwa Sugar
Mabeki ni Shomary Kapombe(Azam),Mohammed Husein Tshabalala(Simba),Hassan Kessy(Yanga),Gadriel Michael(Azam),Andrew Vicent(Yanga),Salim Mbonde(Mtibwa Sugar),Abdi Banda(Simba),na Erasto Nyoni(Azam)
Viungo ni Himid Mao(Azam),Jonas Mkude(Simba),Said Ndemla(Simba),Salum Abubakar "Sure Boy"(Azam),Frank Domayo(Azam),Shiza Kichuya(Simba),Saimon Msuva(Yanga),Mzamil Yassin(Simba),Hassan Kabunda(Mwadui FC),na Farid Mussa(DC Tennerife)
Washambuliaji ni Mbwana Samatta(KRC Genk),Ibrahim Hajib(Simba),Mbarak Yussuf(Mtibwa sugar),Abdulrahman Juma (Ruvu Shooting) na Thomas Ulimwengu(AFC Eskilstuna,Sweden)