Wenger aendeleza sintofahamu kuhusu kuondoka Arsenal

Kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ameendelea kuwa na kigugumizi kuhusu kuondoka klabuni hapo.Kocha huyo raia wa Ufaransa hajatoa tamko rasmi hadi sasa kuhusu kuondoka klabuni hapo licha yamashabiki wa klabu hiyo kumshikinikiza kujiuzuru kutokana na mwenendo wa klabu hiyo kuwa mbovu.Mmoja wa mashabiki wa Arsenal ameibuka na kutoa kauli ambayo amemlinganisha kocha huyo na rais wa zimbambwe Robert Mugabe kutokana na misimamo yake ya kidikteta ambayo imekuwa ikilalamikiwa kwa mda mrefu na wadau wa klabu hiyo.
Kwa misimu 7 mfululizo Wenger ameshindwa kuivusha timu yake kwenda hatua ya robo fainali ya mashindano ya klabu bingwa ulaya akitolewa mara kwa mara katika hatua ya 16 bora.
Licha ya watu wengi kumponda kocha huyo siku za hivi karibuni ameibuka nakutoa kauli yakubeza shtuma kutoka kwa watu wanao mponda.
Hadi sasa hakuna taarifa rasmi yakocha huyo kuachana na klabu hiyo huku kukiwa na uwezekano wa kuongeza mkataba wa miaka kuinoa klabu hiyo