Mbwana Samatta uwanjani leo na klabu yake ya Genk kuikabili Gent katika mechi ya UEROPA league

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Genk Mbwana Samatta leo atakuwa uwanjani na klabu yake ya Genk kuikalibisha Gent katika mechi ya mkondo wa pili ya UEROPA league.
Katika mechi ya mkondo wa kwanza Mbwana Samatta aliisadia klabu yake ya Genk kuibuka na ushindi wa 5-2 ugenini kwa Gent huku akifunga mabao mawili katika mchezo huo.
Genk wataingia uwanjani leo wakiwa na matumaini yakusonga mbele hatua ya robo fainali kutona na matokeo mazuri ya mechi ya kwanza.Ndoto  za kufuzu robo fainali zitazimwa endapo Genk watakubali kufungwa 4-0 katka mchezo wa leo lakini nafasi kubwa yakusonga mbele wanapewa Genk kutokana na timu yao kuimarika zaidi katika mashindano haya.