Kocha wa Chelsea Antonio Conte anamtaka beki wa kulia wa Atalanta Andrea Conti kwa lengo la kuziba pengo hilo baada ya nyota wake Victor Moses kuumia katika mechi na Crystal Palace ambapo Chelsea walipoteza mechi hiyo kwa kukubali kipigo cha 2-1 wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani.
Bosi huyo wa zamani wa Juventus anamfuatilia beki huyo kuona kama atafiti katika kikosi chake ambacho msimu huu kipo katika nafasi nzuri ya kutwaa taji la EPL.