Chelsea wanamfukuzia beki wa Southampton Cedric Soares ilikuimarisha safu yake ya ulinzi ilikujiweka fiti kwa ajili ya msimu ujao.
Chelsea wanataka kukiboresha kikosi chao ilikukabiliana na mapambano ya msimu unaokuja watakapokuwa wanashiliki ligi ya mabingwa ulaya na pia kuhakikisha wanaendelea kuzipa changamoto klabu zinazoshiliki EPL.
Chelsea watakutana na upinzani mkali kutoka kwa Barcelona ambayo nayo inamtaka beki huyo wa kireno ilikuimarisha beki yake ambayo imeonekana kuyumba tangu kuondoka kwa beki wake mkongwe Dan Alves aliyetimkia Juve.