Arsenal yamtengea Sanchez £300,000

Washika mitutu wa jiji la London wamemuwekea mezani nyota wao Alexis Sanchez kitita cha £300,000 kwa wiki ilikumshawishi kuendelea kubaki hapo kutokana na mchango wake kuonekana mkubwa katika kikosi hicho.

Arsenal wanaonekana kutaka kuachana na mfumo wao wa siku zote wakulipa wachezaji wake pesa ndogo safari hii wakionekana kuamua kumwaga pesa ilikukisuka kikosi chake upya.

Licha ya sintofahamu inayoendelea kuhusu mstakabali wa Wenger katika klabu hiyo, viongozi wa Arsenal wapo tayari kumlipa nyota huyo wa Chile kitita cha £300,000 kwa juma ambacho kitamfanya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi katika ligi ya England.

Related Posts: