Klabu ya Chelsea ipo mbioni kukamilisha uhamisho wa kiungo wa Monaco Tiemoue Bakayoko.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka chanzo cha habari cha TuttomercatoWeb inaaminika kwamba the Blues wameshafikia makubaliano ya kumsajiri nyota huyo wa kimataifa kutoka Ufaransa.
Bakayoko amekuwa na msimu mzuri akiwa na timu yake ya Monaco ampbapo timu yake hadi sasa inashikilia usukani wa Ligue 1 kwa jumla ya pointi 71 wakiwaacha mabingwa watetezi PSG waliopo katika nafasi ya pili kwa pointi 3 wakiwa na pointi 68 wakishuka dimbani mara 30 sawa na Monaco.