Lukaku atwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi march Uingereza

Kinara wa kutupia mabao katika ligi kuu ya England msimu huu Romelu Lukaku wa Everton ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi march wa Uingereza.

Tuzo hiyo inakuja baada ya nyota huyo wa kimataifa kutoka Ubelgiji kuonyesha umaridadi wa hali ya juu mwezi march akiipachikia timu yake mabao manne  katika mechi tatu ilizocheza mwezi huo.

Nyota huyo wa Everton ndo anaongoza kwa mabao hadi sasa katika ligi ya England akiwa na mabao (21) akifuatiwa na Harry Kane wa Tottenham mwenye magori(19).

Wachezaji wengine wanaomfukuzia kwa karibu nyota huyo ni Alexis Sanchez kutoka Arsenal mwenye magori(18),Diego Costa kutoka Chelsea mabao (17) pamoja na mshambuliaji wa Man U Zlatan Ibrahimovic mwenye mabao(15).