Man United waitega Barca kwa Neymar

Klabu ya Manchester United imeiingiza katika mtego klabu ya Barcelona baada ya kuitengea klabu hiyo kitita cha uero millioni 200 ilichokuwa ikikitaka ilikumwachia  Neymar.

Chanzo kimoja cha habari kutoka Hispania kimeripoti kuwa United wamesema wako tayari kutoa kiasi hicho  cha pesa ilikumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Brazil.

United wanataka kuendeleza rekodi yao ya kusajili wachezaji kwa bei ghari zaidi  baada ya kufanya hivyo kwa Paul Pogba msimu uliopita na safari hii wameelekeza nguvu zao kwa Neymar ilikumfanya kuwa mchezaji ghari zaidi duniani.