Nyasi kuumia leo kombe la FA Chelsea wakiwakaribisha Spurs

Vigogo wawili wanaokimbizana kwa karibu kuusaka ubingwa wa ligi kuu England Chelsea na Tottenham watakutana leo katika mechi ya nusu fainali kombe la FA .

Chelsea watashuka dimbani leo wakiwa na kumbukumbu na kipigo cha 2-0 kutoka kwa Spurs katika mechi ya raundi ya pili ya EPL iliyochezwa nyumbani kwa Tottenham.

Mechi nyingine itakuwa hapo kesho wakati Arsenal watakapokuwa wanawakaribisha Manchester City katika uwanja wa Emirates kuamua nani ataungana fainali na mshindi wa leo kati ya Chelsea na Spurs