Mbabe wa jiji la Manchester kujulikana leo

Jiji la Manchester usiku huu litasimama kwa mda kushuhudia mchuano mkali unaozikutanisha timu mbili zinazotoka jiji hilo.

Mechi hiyo inayotarajiwa kuchezwa majira ya sa nne kamili kwa majira ya Afrika Mashariki itazikutanisha Manchester City na Manchester United katika uwanja wa Etihad nyumbai kwa Manchester City.

Manchester United watafiri kwenda Etihad wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa 2-1 walipokutana na City katika uwanja wao nyumbani.

City na United zimekutana mara 35 hadi kufikia sasa katika historia yake huku United wakiwafunga  Manchester City katika michezo 17 na City wakishinda michezo 13 pekee huku timu hizo zikitoka sare katika michezo 5.