Pogba kuikosa Manchester derby leo

Kiungo wa Manchester United Paul Pogba atakuwa nje leo wakati timu yake itakapokuwa inamenyana na majirani zao Manchester City katika uwanja wa Etihad.

Pogba ataukosa mtanange huo kutokana na maumivu ya misuli yanayo msumbua licha ya kuchezeshwa katika mechi dhidi ya Burnely siku ya jumapili.

Wengine waliokuwa wakihofiwa kuukosa mchezo huo ni Antonio Valencia na Ander Herrera lakini bosi wa United Jose Mourinho amebainisha kwamba wawili hao watakuwa fiti kuivaa City usiku wa leo