Arda Turan anukia Arsenal


Arsenal wanakaribia kumnasa kiungo wa Barcelona Arda Turan kwa ajili ya kuziba pengo la Mesut Ozil ambaye dalili zinaonesha anaweza kuondoka majira ya joto.

Mchezaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid hana furaha na maisha ya Camp Nou baada ya kushindwa  kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Barcelona na Arsenal wanataka kutumia mwanya huo kumshawishi nyota huyo kutua Emirates majira ya joto