Morata kwenye rada za Manchester United


Manchester United wamewasiliana na viongozi  wa Real Madrid kuhusu upatikanaji wa mshambuliaji Alvaro Morata.

United wapo katika harakati za kutafta mshambuliaji atakaye chukua nafasi ya Msweeden Zlatan Ibrahimovic ambaye amaendamwa na majeraha.

United watapata upinzani kutoka kwa Chelsea ambayo  nayo inamfukuzia mshambuliaji huyo kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Diego Costa ambaye anaweza akaondoka majira ya joto.