Arsenal wanamtaka Emil Forsberg


Arsenal wanataka kumsajili mshambuliaji Emil Forsberg wa RB Leipzig ya Ujerumani katika uhamisho wa majira ya joto.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka The Sun inasemekana kuwa Arsenal wametenga kitita cha pauni millioni 20 kwa ajili ya mshambuliaji huyo na Wenger anataka saini ya mchezaji huyo kwa ajili ya kuja kuongeza makali kwenye safu yake ushambuliaji.