Simba walikata rufaa baada ya kubaini kuwa Kagera Sugar walichezesha mchezaji aliyekuwa na kadi tatu za njano alizozipata mfululizo kinyume na sheria za soka nchini katika mechi iliyochezwa Kaitaba nyumbani kwa Wanankulukumbi ambapo Kagera walishinda 2-1.
Akiongea na wanahabari usiku wa April 13 mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Ahmed Yahya amesema kwamba kamati imebaini kosa hilo lilifanywa kweli na Kagera Sugar na hivyo klabu hiyo itapokonywa ushindi ilioupata katika mechi hiyo.
Simba wanafikisha pointi 61 baada ya ushindi huo wakiwa wamecheza mechi 26 na kuwaacha kwa tofauti ya pointi 5 watani wao wa jadi Yanga waliocheza mechi 25.