Messi kusaini mkataba mpya


Nyota wa Barcelona Lionel Messi anakaribia kusaini mkataba mpya na klabu yake wakati mkataba wake wa sasa ukielekea ukingoni.

Wiki chache zilizopita  Messi alilipotiwa kuigomea Barcelona kuongeza mkataba mpya lakini makamu wa rais wa klabu ya Barcelona Jordi Mestre ameviambia vyombo wa habari kuwa mazungumzo na nyota huyo wa kimataifa wa Argentina yanaendelea vizuri na kwamba siku si nyingi nyota huyo atasaini mkataba mpya.

Mkataba wa Messi unaisha 2018 na Barcelona wanataka kumsainisha mkataba mpya ilikuhakikisha kuwa anaendelea kubakia Camp Nou.

Messi amekuwa akihusishwa na mipango ya kuungana na kocha wake wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola anayeinoa Man City hivyo Barca wanajaribu kutumia mbinu zote kuhakikisha hawampotezi staa huyo.