Arsenal kukumbana na kigingi kumpata Kylian Mbappe

Matumaini ya Arsenal kumnasa mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe yanaonekana kukwama baada ya Monaco kutangaza dau kubwa ambalo linaonekana Arsenal hawataweza kutoa kulingana na desturi ya uongozi wa klabu hiyo.
Monaco wamesema watakuwa tayari kumuuza mchezaji huyo kwa timu pekee itakayokuwa na kiasi cha pauni millioni 130 ambapo dau hilo linaonekana mlima mkubwa kwa Arsenal kuupanda katika kusaka saini ya mshambuliaji huyo.
Mbappe mwenye umri wa miaka 18 anawindwa pia na klabu za Real Madrid na Man United ambapo Man United wanaonekana kuelekea kuzipiku timu zingine zinazomtaka kinda huyo baada ya kuitengea Monaco kitita cha pauni million 110 ilikumnasa mchezaji huyo