Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid James Rodriguez anapotiwa kuwa anaweza kujiunga na klabu ya Liverpool katika uhamisho wa majira ya joto endapo klabu hiyo itafanikiwa kumaliza katika nafasi za juu itakayo iwezesha klabu hiyo kushiriki mashindano ya klabu bingwa msimu ujao.
Nyota huyo raia wa Columbia anataka kuachana na klabu yake ya Madrid baada ya kukosa namba ya kudumu katika kikosi kinachonolewa na kiungo wa zamani wa Ufaransa.Katika msimu huu ameanza mechi saba pekee za la liga ikionekana kocha wa timu hiyo kutoridhishwa na kiwango cha mchezaji huyo.