Arsenal na Tottenham zapigana vikumbo kwa nyota wa Sampdoria

Arsenal na Tottenham zimeingia katika vita ya kumuwania mshambuliaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech na klabu ya Sampdoria Patrick Schick.

Taarifa kutoka gazeti la Daily Mail zimeripoti kwamba wakala wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alikuwa anatarajiwa kufanya mazungumzo na klabu hizo siku ya jumatano.
Nyota huyo anatajwa kugharimu kiasi cha pesa pauni millioni 12 kwa timu yeyote ambayo itahitaji kumsajili.