Klabu ya Chelsea inamsaka nyota wa klabu ya Arsenal Alexis Sanchez ambaye ameripotiwa kuwa ataihama Arsenal katika majira ya joto.
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amemtaja winga huyo wa kimataifa wa Chile katika majina ya wachezaji ambao anataka kuwasajiri katika uhamisho wa majira ya joto.
Alexis ambaye anaonekana kukerwa na mwenendo wa klabu ya Arsenal huenda akajiunga na miamba hiyo kutoka London baada ya klabu hiyo kumtengea dau nono ilikumshawishi kujiunga na miamba hiyo.
Licha ya Chelsea kujipanga kumnasa nyota huyo klabu ya Arsenal imeripotiwa kukataa kumuuza mchezaji huyo katika timu za Uingereza na huenda sasa klabu za PSG ,Juventus na Inter Milan zikapata mwanya wa kumnasa nyota huyo baada ya klabu hizo kuripotiwa kumtaka winga huyo.