Miamba hiyo ya La Liga imekuwa ikimsaka nyota huyo kwa mda mrefu na sasa inaonekana kushinda mbio za kumnasa mchezaji huyo.
Madrid wametenga dau la pauni millioni 100 ilikuhakikisha wanampata mchezaji huyo ambaye anaonekana atakuwa msaada katika kikosi cha kocha wa timu hiyo Zinadine Zidane ambaye anataka kuimarisha kikosi chake.
Licha ya Chelsea kutaka kumsainisha mkataba mpya nyota huyo imeripotiwa nyota huyo kutoka Ubelgiji anajiandaa kuihama Chelsea na tayari inasemekana anajifunza kihispaniola huku Madrid ikiwa inaendelea kuweka sawa mahesabu yake yakumnasa nyota huyo gazeti la Metro limeripoti