City waichokoza Barcelona kwa Messi


Man City wameitengea Barcelona kitita cha pauni millioni 200 kwa ajiri ya kumchukua mshambuliaji wake Lionel Messi katika uhamisho wa majira ya joto.Imepotiwa kuwa kitita hicho cha pesa tayari ashakabidhiwa kocha wa Man City Pep Guardiola ili kuhakikisha kwamba anamshawishi mchezaji huyo kujiunga na Man City.

Taarifa kutoka Sunday Express zinadai kwamba City wanauhakika watampata nyota huyo wa kimataifa wa Argentina kulingana na klabu ya Barca kushindwa kumpa kiasi cha pesa cha mshahara anotaka nyota huyo.


Siku za hivi karibuni baada ya Guardiola kutua Man City amekuwa akitaka kumsajili mchezaji huyo ambaye amemfundisha alipokuwa akiinoa Barca kabla hajatimkia Ujerumani nasafari hii uongozi wa klabu ya Man City umemkabidhi kitita hicho ilikuona kama ataweza kumshawishi mchezaji huyo kujuimuika naye klabuni hapo.

Related Posts: