Arsenal yaandaa dau nono kwa Benzema

Arsenal wanataka kumsajili  mshambuliaji wa Real Madrid Kalim Benzema katika uhamisho wa majira ya joto.

Arsenal wameripotiwa kumtengea mshambuliaji huyo kitita cha £300,000  kwa wiki endapo atakubali kujiunga na klabu hiyo.

The Gunners wapo katika mipango ya kutafta mbadala wa Alexis ambaye mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya yanaonekana kukwama  mara kwa mara.