Jonh Terry kuondokeaa Chelsea mwishoni mwa msimu

Nahodha wa mda mrefu wa Chelsea Jonh Terry ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa hizo zimekuja baada ya beki huyo na Chelsea kwa pamoja kutangaza kuwa nyota huyo atatimka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

Terry alijiunga na Chelsea mwaka 1995 akitokea West ham United  na ameichezea klabu hiyo mechi 713 hadi sasa.

Beki huyo anakuwa mchezaji wa tatu kuichezea mechi nyingi zaidi klabu hiyo pia akivunja rekodi ya kuingoza klabu akiwa nahodha mara 578.