Everton waitaka Chelsea kutoa Euro millioni 100 kwa Lukaku

Everton wameitaka Chelsea kutoa kiasi cha pesa cha euro million 100 kama wantaka kumpata mshambuliaji wake Romelu Lukaku.

The Toffees wamesisitiza kuwa hawatamwachia nyota huyo kwa pesa chini ya euro mia kujiunga na Chelsea na klabu zingine zinazomtaka mshambuliaji huyo.

Lukaku hajasaini mkataba mpya na Everton hadi sasa na huenda akatimka klabuni hapo endapo timu zitakuabli kutoa kiasi cha pesa ambacho Everton wanakitaka.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa ubelgiji anaongoza kwa kuzifumania nyavu za timu pinzani katika ligi kuu ya Uingereza akiwa na mabao 24 hadi sasa.