United yamfungia kazi Barkley

Manchester United wameingia vitani kuisaka saini ya nyota  wa Everton Ross Barkley ambaye nasuasua kuisani mkataba mpya na Everton.

Raia huyo wa Uingereza amekataa kusaini mkataba mpya na Everton na United wanataka kutumia nafasi hiyo kumnasa nyota huyo katika majira ya joto.

Mkataba wa sasa wa nyota huyo umebakiza mwaka mmoja kumalizika hivyo kugoma kwake kusaini mkataba mpya kunaweza kukavifungulia mlango vilabu vya Ulaya kumsajili mchezaji huyo