Sanchez kuuzwa PSG endapo hatasini mkataba mpya Emirates

Arsenal watamuuza Sanchez kwenda PSG endapo makubaliano ya kuongeza mkataba hayatafikiwa,kwa mjibu wa The Sun.

Taarifa hizo zimetolewa na uongozi wa Arsenal baada ya mipango ya kumbakisha nyota huyo Emirates kuonekana kusuasua.

Vigogo wa Arsenal wamesema hawatamuuza nyota huyo kwa timu yeyote ya England badala yake watamuuza kwenda PSG kama itashindikana kumshawishi kuongeza mkataba mpya.

Manchester City na Chelsea zinamfukuzia nyota huyo kutoka Chile lakini huenda zikaikosa saini yake kama Arsenal watashikilia msimamo wao wa kutomuuza nyota huyo kwa vilabu vya Uingereza.