Atletico Madrid wanamtaka Cesc Fabregas

Atletico Madrid wanataka kumsajili kiungo wa zamani wa Arsenal Cesc Fabregas katika uhamishi wa wachezaji majira ya joto.

Nyota huyo wa Kihispaniola ameshindwa kupata namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Chelsea kinachonolewa na muitaliano Antonio Conte hivyo anaweza akarejea nyumbani kukipiga katika miamba hiyo.