Bale kuikosa mechi ya Bayern Munich usiku wa leo

Staa wa Real Madrid Gareth Bale ataikosa mechi ya mkondo wa pili ya Uefa hatua ya robo fainali kati ya timu yake ya Real Madrid na Bayern Munich usiku wa leo kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Bale huenda akaikosa pia mechi ya El clasico wiki hii kama afya yake haitaimalika mapema kuelekea mchezo huo.

Kocha wa Madrid Zinedine Zidane amesema hatamchezesha winga huyo katika mechi ya leo ilikumpa nafasi kupona vizuri majeraha yake.

Madrid watawakaribisha Bayern katika uwanja wao wa nyumbani wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa 2-1 walioupata ugenini kwa Bayern wiki iliyopita.