Lewandowski alikaribia kujiunga Real Madrid 2014

Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski imebainika kuwa alikaribia kujiunga na Real Madrid katika uhamisho wa majira ya joto 2014.

Madrid walitaka kumsajili  nyota huyo kwa euro millioni 17 lakini waliamua kuachana naye na badala yake kuelekeza nguvu kwa Kalim Benzema.

Nyota huyo raia wa Poland alijiunga na Bayern kwa uhamisho wa bure baada ya mkataba wake kuisha  na iliyokuwa timu yake Borrussia Dortmund.