Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 amekuwa katika kiwango bora zaidi msimu huu na kuzivutia timu mbalimbali za Ulaya kuitaka saini yake.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza amefunga mabao 16 hadi sasa katika Ligi kuu ya England akiachwa nyuma mabao 8 na kinara wa mabao wa Ligi hiyo Romelu Lukaku wa Everton.